Friday, January 24, 2020

Majukumu na Kazi

 Majukumu, kazi na muundo wa SUMATRA

1. UTANGULIZI
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 9 ya mwaka 2001. Mamlaka ilianza kazi kisheria tarehe 20.08.2004, kwa Tangazo la Serikali Na. 297/2004.

Mamlaka inasimamia udhibiti wa soko la usafirishaji wa nchi kavu na majini ikiwa ni pamoja na usalama na utunzaji wa mazingira.

2. MAJUKUMU YA MAMLAKA

2.1 Kuhimiza/Kukuza ushindani na ufanisi katika soko la usafirishaji wa nchi kavu na majini.
2.2 Kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma
2.3 Kulinda na kujenga mazingira ya kuvutia kwa watoa huduma.
2.4 Kuendeleza na kuhakikisha kuwa huduma za usafirishaji zinakidhi mahitaji ya watumiaji ikiwa ni pamoja na wenye kipato cha chini na wasiojiweza.
2.5 Kuwaelimisha watumiaji huduma na Wananchi kwa ujumla kuhusu sekta zinazodhibitiwa ikiwa ni pamoja na:

 •  Haki na wajibu wa watumiaji na watoa huduma na bidhaa.
 •  Jinsi ya kuwakilisha malalamiko/migongano na utatuzi wake.
 •  Kazi na majukumu ya Mamlaka.


2.6 Kuboresha na kusimamia viwango vya usalama katika sekta zinazosimamiwa na kudhibitiwa na Mamlaka.
2.7 Kuhakikisha kuwa watoa huduma na watumiaji wanalinda na kutunza mazingira.

3. KAZI ZA MAMLAKA

3.1 Kutekeleza majukumu yalioko chini yake kwa mujibu wa Sheria za kisekta.
3.2 Kutoa leseni kwa watoa huduma.
3.3 Kuweka viwango na masharti mengine kwa watoa huduma.
3.4 Kusimamia utendaji kazi wa sekta zilizoko chini ya Mamlaka.
3.5 Kuratibu na kuwezesha utatuzi wa malalamiko na migongano katika soko la usafirishaji.
3.6 Kutoa taarifa mbalimbali kuhusu sekta zinazodhibitiwa na Mamlaka na kukuza ushirikiano na Wakala zingine za Serikali.
3.7 Kuchukua na kuendelea kutekeleza majukumu ya iliyokuwa Tanzania Central Freight Bureau (TCFB).
3.8 Kusimamia na kudhibiti usalama wa usafirishaji wa majini.

4. MUUNDO WA MAMLAKA


Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) ni Mamlaka ambayo iko huru. Mamlaka inaongozwa na Bodi ya Wakurugenzi.

Menejiment ya Mamlaka inaongozwa na Mkurugenzi Mkuu ambaye husimamia shughuli za kila siku za Mamlaka.

Mamlaka ina Idara/Kurungenzi nane ambazo ni:-

 •  Idara ya udhibiti wa Bandarini na usafiri wa majini (Ports and Shipping Services Regulation)
 •  Idara ya Udhibiti wa usafiri kwa njia ya Reli (Railways Regulation)
 •  Idara ya Udhibiti wa usafari kwa njia ya Barabara ( Road Transport Regulation) 
 • Idara ya Udhibiti wa usalama na Ulinzi na usafiri wa Majini (Maritime Safety and security)
 •  Idara ya udhibiti wa Uchumi (Economic Regulation)
 • Idara ya Huduma za Mamlaka (Corporate Affairs)
 • Idara ya Huduma za Ukaguzi ( Performance Audit)
 •  Idara ya Huduma za Kisheria (Legal Services)

Vile vile Mamlaka ina Ofisi za mikoa kama ifuatavyo:-

1. Dar es Salaam

5. Mbeya

9. Kagera

13. Ruvuma

2. Tanga

6. Mwanza

10. Kigoma

14. Shinyanga

3. Mtwara

7. Kilimanjaro

11. Mara

15. Tabora

4. Dodoma

8. Arusha

12. Rukwa

16. Iringa

 

 

 

 

 

 

Makao Makuu


Makao makuu ya Mamlaka yapo Dar es Salaam katika jengo la Mawasiliano House lililopo kwenye kona ya barabara za Ali Hassan Mwinyi na Nkomo.