Friday, December 13, 2019

Sherehe ya Uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi Yaendayo Haraka

 

 

 

 

 

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 


SHEREHE YA UZINDUZI WA MIUNDOMBINU NA HUDUMA ZA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART) ULIOFANYIKA  JUMATANO TAREHE 25 JANUARI 2017, AMBAPO RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI ALIKUWA MGENI RASMI.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akihutubia katika sherehe ya Uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka (DART)

 

 


 
Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Afrika Bw. Makhtar Diop (wa kulia), wakielekea kuzindua mradi wa DART kwa kufungua pazia la jiwe la msingi, ambapo benki ya dunia ndio wahisani wakuu wa mradi huo

 

 

 

Rais Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Afrika Bw. Makhtar Diop wakizindua rasmi miundombinu ya mradi DART kwa kufungua pazia kwa pamoja. Pembeni ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akishuhudia uzinduzi huo

 

 

Rais Magufuli akipongezana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa mara baada ya uzinduzi wa mradi wa DART

 

 

 

Rais Magufuli akipongezana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Afrika Bw. Makhtar Diop mara baada ya uzinduzi wa mradi wa DART

 

 

Rais Magufuli akimwita Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba ili wapige picha ya ukumbusho pamoja

 

 

Rais Magufuli akishikana mikono na viongozi na wadau mbalimbali walioshiriki kwa njia moja au nyingine katika kufanikisha mradi wa DART mara baada ya kuzindua mradi huo


 

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Afrika Bw. Makhtar Diop akipanda mti ikiwa ni ukumbusho wa uzinduzi wa mradi huo wa DART

 

 


Rais Magufuli na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Afrika Bw. Makhtar Diop wakizindua mashine za kukagua tiketi za mradi wa DART

 

 

 

Rais Magufuli katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mradi wa DART pembeni mwa moja ya Mabasi Yaendayo Haraka yanayotumika katika mradi huo

 

 

 

Rais Magufuli akiendesha moja ya Mabasi Yaendayo Haraka baada ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za DART